Jobs in Tanzania

Walioitwa Kazini Utumishi August 2025

Hii hapa orodha ya Majina ya walioitwa kazini utumishi afya, walimu na kada mbalimbali leo Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anawataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 05/09/2024 na tarehe 28/06/2025 kuwa matokeo ya waliofaulu yameorodheshwa kwenye tangazo hili.

Nafasi za Kazi Ajira Portal

Orodha hii pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

Kupata Barua za Kupangiwa Kituo cha Kazi

  • Wasailiwa wote waliofaulu na kupangiwa vituo vya kazi watapata barua kupitia akaunti zao za Ajira Portal kwenye sehemu ya My Applications.
  • Watahitajika kupakua (Download) na kuchapisha (Print) barua hizo.
  • Wakiwa na barua hizo, wanapaswa kuripoti katika vituo walivyopangiwa.

Maelekezo ya Kuripoti Kazini

  • Waombaji kazi wanapaswa kuripoti kwa mwajiri ndani ya muda uliobainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi.
  • Wakiwa na vyeti halisi vya masomo kuanzia Kidato cha Nne na kuendelea kwa ajili ya uhakiki kabla ya kupewa barua ya ajira rasmi.

Taarifa kwa Wasiofaulu
Kwa wale ambao majina yao hayapo kwenye tangazo hili, watambue kuwa hawakufaulu usaili au hawakupata nafasi. Wanahimizwa kuomba tena mara nafasi mpya zitakapotangazwa.

Soma zaidi:

Leave a Comment