Tarehe 5 Aprili 2025, Wizara ya TAMISEMI ilitoa taarifa rasmi kwa wanafunzi wa kidato cha tano 2025 waliopangiwa shule na combination kwamba wanaweza kuomba mabadiliko ya tahasusi (combination) selform.tamisemi.go.tz, Tahasusi (Combination) Bora Kidato cha tano selform 2025, kupitia mfumo rasmi. Hii imezingatia maombi ya wanafunzi wengi waliopangiwa combination zisizolingana na matamanio yao au uwezo wao wa kitaaluma. Combination Bora za Kidato cha Tano 2025 PDF
Kwa nini ni muhimu kubadilisha combination mapema?
- Kubadilisha kwa wakati kunaepusha kusoma combination usiyoimudu wala kuipenda.
- Unapata nafasi ya kuchagua combination yenye fursa halisi za ajira na maendeleo ya kitaaluma.
- Ni nafasi ya kurekebisha mwelekeo wa maisha yako kwa maamuzi sahihi.
Orodha ya Combination Bora za Kuchagua Mwaka 2025 (Zenye Ajira na Fursa)
Ninapendekeza kuzingatia combination zifuatazo ikiwa unafikiria kubadilisha kupitia TAMISEMI:
1. PCB – Kwa Ndoto za Udaktari, Uuguzi na Afya
Ajira: Daktari, Mtaalamu wa Maabara, Mtafiti wa Afya, Afisa Afya ya Umma.
2. PCM – Kwa Wahandisi, Wanasayansi wa Teknolojia, na Hesabu
Ajira: Software Developer, Mhandisi, Data Analyst, ICT Expert.
3. EGM – Kwa Uchumi, Takwimu na Mipango
Ajira: Mchumi, GIS Expert, Mtaalamu wa Takwimu, Urban Planner.
4. CBG – Kwa Sayansi ya Maisha, Kilimo na Mazingira
Ajira: Afisa Mazingira, Mtafiti wa Viumbe, Mkulima wa Kibiashara.
5. HGL – Kwa Sheria, Habari, Diplomasia
Ajira: Mwanasheria, Diplomat, Mwandishi, Mwalimu wa Historia na Lugha.
6. HKL – Kwa Lugha, Elimu na Uandishi
Ajira: Mwandishi, Mkufunzi, Mhariri, Mkalimani, Mwalimu.
Unafaa Kumbuka Haya Kabla ya Kubadilisha Combination
- Angalia matokeo yako ya kidato cha nne – chagua combination inayolingana na uwezo wako.
- Tathmini ndoto zako za maisha – usifuate mkumbo, fuata wewe.
- Zingatia fursa za ajira na kozi za vyuo vikuu.
- Fuata utaratibu rasmi wa TAMISEMI kwa kubadilisha combination kupitia selform.tamisemi.go.tz.
Jinsi ya Kubadilisha Tahasusi Kupitia TAMISEMI (Hatua kwa Hatua)
- Tembelea tovuti ya TAMISEMI: https://selform.tamisemi.go.tz
- Ingia kwa kutumia Namba yako ya mtihani na Mwaka wa kumaliza (2024).
- Nenda kwenye sehemu ya “Badilisha Combination”.
- Chagua combination mpya unayotaka kulingana na ufaulu wako.
- Hakikisha unahifadhi mabadiliko na chapisha risiti ya uthibitisho.
Kumbuka: Fursa hii ni kwa muda mfupi tu. Hakikisha unafanya mabadiliko kabla ya muda wa mwisho uliotangazwa.
Hitimisho: Chagua Combination kwa Maarifa, Sio kwa Bahati Nasibu
Wanafunzi wengi wamewahi kusema, “Laiti ningejua mapema…” Usisubiri kujuta. TAMISEMI imekupa fursa ya kubadilisha tahasusi—itendee haki kwa kufanya uamuzi unaoendana na ndoto zako, uwezo wako, na fursa zilizopo.
SOMA ZAIDI: