Hili hapa tangazo la nafasi za kazi Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na UNEP, UNHCR, Sekretarieti ya Mkoa wa Kigoma, NEMC na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), wamezindua mradi mpya unaoitwa “Kujenga Uhimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi Mkoa wa Kigoma.”
Mradi huu unafadhiliwa na Green Climate Fund (GCF) kupitia UNEP na unalenga kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika mkoa wa Kigoma.
Mradi huu utaanza rasmi mwaka 2024 hadi 2028, na utatekelezwa katika wilaya za Kasulu, Kibondo na Kakonko. Lengo kuu ni kusaidia jamii ziwe na uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia matumizi bora ya ardhi, uhifadhi wa rasilimali za asili, na kilimo rafiki kwa mazingira.
Kupitia mradi huu, Ofisi ya Makamu wa Rais inakaribisha Watanzania wenye sifa kutuma maombi ya kazi mbalimbali zitakazotekelezwa ndani ya muda wa miaka mitano ya mradi huu.
Ajira mpya Ofisi ya Makamu wa Rais zilizotangazwa
SOMA ZAIDI:–