Admission

Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Jeshi la Polisi 2025

Tangazo Rasmi la Tarehe 23 Aprili 2025 Jeshi la Polisi limetoa tangazo rasmi kwa vijana wote waliotuma maombi ya kujiunga na Jeshi hilo kupitia mfumo wa Tanzania Police Force Recruitment Portal. walioitwa kwenye usaili jeshi la polisi, usaili jeshi la polisi 2025, tangazo la usaili jeshi la polisi PDF, Tangazo hili linahusu majina ya waliochaguliwa kwenda kwenye usaili pamoja na ratiba kamili ya mchakato huo. majina ya walioitwa kwenye usaili jeshi la polisi 2025

Nafasi za Kazi Ajira Portal

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, usaili wa Jeshi la Polisi 2025 utaanza tarehe 28 Aprili 2025 saa 1:00 asubuhi na kuendelea hadi 11 Mei 2025. Usaili utafanyika katika maeneo tofauti kulingana na aina ya elimu ya mwombaji.

Usaili kwa Waliohitimu Shahada, Stashahada na Astashahada

Kwa waombaji wenye elimu ya juu (Degree, Diploma, na Certificate), usaili wote utafanyika jijini Dar es Salaam katika uwanja wa gwaride wa Kambi ya Polisi (Police Barracks), uliopo barabara ya Kilwa, nyuma ya Kituo cha Polisi Kilwa Road.

Usaili kwa Waliohitimu Kidato cha Nne na Sita

Kwa waombaji wa ngazi ya elimu ya sekondari (Form Four na Form Six), usaili utafanyika katika mikoa waliyoiainisha wakati wa kutuma maombi. Wahusika wanapaswa kufika kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa husika.

Usaili kwa Walioitwa Kutoka Zanzibar

Kwa waombaji walioko Zanzibar, usaili utafanyika katika maeneo yafuatayo:

  • Unguja: Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (eneo la Ziwani)
  • Pemba: Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba (eneo la Chakechake)

Vitu vya Muhimu kwa Msailiwa Kufika Navyo

Kila msailiwa anapaswa kufika kwenye eneo la usaili akiwa na:

  • Vyeti halisi vya taaluma (Academic Certificates)
  • Cheti cha kuzaliwa
  • Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya usajili ya NIDA
  • Nguo na viatu vya michezo kwa ajili ya mazoezi ya usaili

Msailiwa yeyote hatakayeripoti baada ya tarehe 28 Aprili 2025 hatapokelewa.

Orodha ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Polisi 2025

Majina yote ya waliochaguliwa kwa ajili ya usaili yameambatanishwa rasmi pamoja na tangazo hili. Ili kupata orodha kamili kwa urahisi, tembelea tovuti ya AjiraTimes.com na utafute kwa kutumia jina lako au namba ya maombi.

PAKUA ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI JESHI LA POLISI HAPA

Leave a Comment