Hii hapa orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili Muhimbili (MUHAS), Makamu Mkuu wa Chuo, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote waliotuma maombi kuwa usaili utafanyika kuanzia tarehe 19 Mei 2025 hadi 20 Mei 2025. Baada ya usaili, waombaji watakaofaulu watapangiwa vituo vya kazi kulingana na mahitaji.
Nafasi za Kazi
Ajira Portal
Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa
- Ratiba ya Usaili: Usaili utaanza kwa tarehe na muda kama ilivyoainishwa katika tangazo husika. Kila kada imepangiwa eneo lake la kufanyia usaili.
- Barakoa (Mask): Ni lazima kwa kila msailiwa kuvaa barakoa wakati wote wa usaili.
- Utambulisho: Msailiwa anatakiwa kuwa na kitambulisho halali kwa ajili ya utambuzi. Vitambulisho vinavyokubalika ni:
- Kitambulisho cha Mkazi
- Kitambulisho cha Mpiga Kura
- Kitambulisho cha Kazi
- Kitambulisho cha Uraia
- Hati ya Kusafiria
- Vyet Halisi: Wasailiwa wote watalazimika kuwasilisha vyeti halisi vyao, ambavyo ni:
- Cheti cha Kuzaliwa
- Cheti cha Kidato cha IV na VI (endapo vinahitajika)
- Diploma/Stashahada
- Stashahada ya Juu
- Shahada na vyeti vya juu zaidi, kulingana na sifa za mwombaji
- HAKUBALIKI: Hati zifuatazo hazitakubaliwa:
- Testimonials
- Statement of Results
- Provisional Results
- Slips za matokeo ya Kidato cha IV na VI
Msailiwa atakayeleta nyaraka hizi hataruhusiwa kuendelea na usaili.
- Gharama Binafsi: Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi kwa kipindi chote cha usaili.
- Uzingatiaji wa Ratiba: Kila msailiwa anatakiwa kuzingatia tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
- Waliosoma Nje ya Nchi: Waombaji waliopata elimu nje ya Tanzania lazima wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika kama:
- TCU
- NACTE
- NECTA
- Wasioitwa kwenye Usaili: Waombaji ambao majina yao hayajaorodheshwa katika tangazo hili wanatakiwa kufahamu kuwa hawakukidhi vigezo. Hata hivyo, wanahimizwa kuendelea kuomba nafasi zitakazotangazwa siku zijazo.
- Usajili wa Kada za Kitaaluma: Kwa kada zinazohitaji usajili wa kitaaluma, waombaji waje na vyeti halisi vya usajili pamoja na leseni ya kufanya kazi kutoka bodi husika.
- Namba ya Mtihani: Kila msailiwa anatakiwa kuingia kwenye akaunti yake (iliyotumika wakati wa kuomba kazi) na kunakili namba ya mtihani, kwani namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.
MUHIMU: Tafadhali zingatia kwa makini maelekezo yote yaliyotolewa ili kuepuka usumbufu au kuondolewa kwenye mchakato wa usaili.
Kuitwa kwenye Usaili Muhimbili (MUHAS)
SOMA ZAIDI:-