Ikiwa unajiuliza kama jina lako limeitwa kwenye usaili wa oral au wa vitendo TRA 2025, habari njema ni kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa rasmi orodha ya waliochaguliwa kuendelea kwenye hatua inayofuata ya usaili. Taarifa hii imetolewa leo tarehe 25 Aprili 2025, ikijumuisha majina ya walioitwa kwenye usaili ufuatao TRA baada ya kufanikisha hatua ya usaili wa maandishi. Majina ya walioitwa kwenye usaili wa vitendo TRA 2025, TRA oral interview 2025, Usaili TRA 2025 PDF
Kwa zaidi ya waombaji 78,000 walioshiriki katika usaili wa maandishi, wanaoendelea kwa hatua ya usaili wa ora na vitendo TRA 2025 sasa wanapaswa kujiandaa kwa mahojiano na usaili wa vitendo ambao utaanza mapema mwezi Mei 2025.
Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili wa Oral na Vitendo TRA 2025 (PDF)
Kwa mujibu wa taarifa kutoka TRA, kupitia Mshauri Elekezi – NBAA, majina ya walioitwa kwenye usaili wa oral na vitendo TRA 2025 PDF yametolewa rasmi.
Majina haya yanapatikana kwenye: Tovuti rasmi ya TRA, Chanzo bora cha matangazo ya ajira, orodha za usaili na updates zote za ajira Tanzania. Kwa kupakua orodha kamili ya walioitwa kwenye usaili ufuatao TRA 2025, tembelea moja kwa moja: www.ajiratimes.com
Ratiba Kamili ya Usaili wa Ora na Vitendo TRA 2025
TRA imetoa ratiba rasmi ya usaili ufuatao kwa mwaka 2025 kama ifuatavyo:
Aina ya Usaili | Tarehe |
---|---|
Usaili wa Vitendo (Madereva, Waandishi) | 2 hadi 4 Mei 2025 |
Usaili wa Mahojiano (Oral Interview) | 7 hadi 9 Mei 2025 |
Matokeo ya Usaili wa Mahojiano | 18 Mei 2025 |
Mafunzo Elekezi kwa Waajiriwa Wapya | 22 Mei hadi 2 Juni 2025 |
Ni muhimu kufuatilia kwa karibu ratiba hii ili usiache nafasi yako ya ajira TRA kupita.
TRA: Mchakato wa Usaili Unaendeshwa na NBAA kwa Uwiano wa Haki
TRA imeeleza kuwa mchakato mzima wa usaili (kuanzia maandishi, vitendo hadi mahojiano) unasimamiwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu – NBAA, huku TRA ikiwa ni msimamizi wa juu pekee.
“Mamlaka ya Mapato Tanzania haina mamlaka ya kutunga wala kusahihisha mitihani ya usaili – jukumu hilo ni la Mshauri Elekezi,”
taarifa rasmi imeeleza. Hii inalenga kuhakikisha kwamba mchakato wa usaili ni wa haki, wazi na usio na upendeleo wowote
SOMA ZAIDI:-