Interview

Walioitwa kwenye Usaili Wakala wa Vipimo (WMA)

Hii hapa orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) anapenda kuwataarifu waombaji wa nafasi ya kazi ya Dereva Daraja la II kuwa usaili utafanyika kwa hatua mbalimbali kama ifuatavyo:

Nafasi za Kazi Ajira Portal

Ratiba ya Usaili

  • Usaili wa Kuandika/Mchujo:
    Tarehe: 17 Mei 2025
    Mahali: Ukumbi wa Nyerere (Lecture Theatre 2), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
  • Usaili wa Vitendo:
    Tarehe: 19 – 20 Mei 2025
    Mahali: Chuo cha VETA, Yombo Buza – Dar es Salaam
  • Usaili wa Mahojiano:
    Tarehe: 22 Mei 2025
    Mahali: Ofisi za Wakala wa Vipimo, Makao Makuu – Dar es Salaam

Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa

  1. Hudhuria kwa Muda Sahihi: Usaili utaanza kwa tarehe na muda ulioainishwa, katika maeneo yaliyotajwa. Hakikisha unawahi.
  2. Kitambulisho Halali: Kila msailiwa anatakiwa kuja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi. Vitambulisho vinavyokubalika ni:
    • Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
    • Kitambulisho cha Mpiga Kura
    • Leseni ya Udereva
    • Hati ya Kusafiria
    • Kitambulisho cha Kazi
    • Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji/Shehia
  3. Vyet Halisi: Leta vyeti halisi vifuatavyo:
    • Cheti cha Kuzaliwa
    • Cheti cha Kidato cha IV na VI (ikiwa husika)
    • Cheti cha Udereva
    • Leseni ya Udereva
  4. HAKUBALIKI: Hati za matokeo (Statement of Results), matokeo ya muda (Provisional Results), Testimonials na Form V/VI Results Slips hazitakubaliwa. Msailiwa atakayewasilisha nyaraka hizi hataruhusiwa kuendelea na usaili.
  5. Gharama: Kila msailiwa atagharamia mwenyewe masuala ya usafiri, chakula na malazi.
  6. Uhakiki kwa Waliosoma Nje: Waombaji waliopata elimu nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika kama NACTVET, TCU au NECTA.
  7. Wasioitwa kwenye Usaili: Waombaji ambao majina yao hayakutajwa kwenye tangazo hili wanatakiwa kufahamu kuwa hawakukidhi vigezo vya awali. Hata hivyo, wanahimizwa kuendelea kuomba nafasi nyingine zitakapotangazwa.
  8. Mamlaka ya Kuondoa Wasio na Sifa: Msailiwa yeyote atakayeshindwa kuwasilisha nyaraka kamili kama zilivyoelekezwa katika vipengele 2, 3, 4 na 6 hatashiriki katika hatua yoyote ya usaili.

Kuitwa kwenye usaili Wakala wa Vipimo (WMA)

SOMA ZAIDI:-

  1. Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026
  2. Ajira Portal 2025: Uhuishaji wa Taarifa za Wasailiwa
  3. Walioitwa kwenye Semina Tume ya Uchaguzi (INEC)
  4. Matokeo ya Usaili wa Kuandika TRA 2025 Tazama Hapa

Leave a Comment